LHRC HQ: Justice Lugakingira House
+255 22 2773038 / +255 22 2773048

MUHTASARI WA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA 2017

  • MUHTASARI WA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA 2017

MUHTASARI WA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA 2017


Organization Report

Report attachment

Download

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekua kikiandaa ripoti kuhusu biashara na haki za binadamu tangu mwaka 2012. Hivyo, hii ni ripoti ya sita kutengenezwa, ikiangazia uzingatiaji wa makampuni na biashara nyingine wa sheria na viwango vya kazi, wajibu wa makampuni kuheshimu haki za binadamu, wajibu wa Serikali kulinda haki za binadamu na upatikanaji wa nafuu pale ambapo haki za binadamu katika sekta ya biashara zimevunjwa. Ripoti hii imejikita upande wa Tanzania Bara pekee.
Taarifa zilizotumika kuandaa ripoti hii zilikusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, ikiwemo ufatifi uliofanyika katika mikoa 15 ya Tanzania Bara, ambapo makampuni 55 yalitembelewa, ukihusisha washiriki 1,067. Taarifa pia zilipatikana kutoka kwa wanajamii, maafisa za vyama vya wafanyakazi, maafisa wa mamlaka za usimamizi na udhibiti katika sekta ya biashara na ripoti mbalimbali za taasisi za Serikali, asasi za kiraia pamoja na vyombo vya habari.
Lengo kubwa la ripoti hii ni kuonesha hali ya biashara na haki za binadamu kwa mwaka 2017 kwa upande wa Tanzania Bara, ikionyesha ni kwa namna gani makampuni yaliweza kuzingatia sheria za kazi, ardhi na mazingira; na namna gani makampuni hayo yaliheshimu au kuvunja haki za binadamu. Ripoti hii itatumika kama nyenzo ya kuboresha haki za binadamu katika sekta ya biashara nchini.

Muundo wa Ripoti
Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara 2017 ina jumla ya sura nane. Sura ya Kwanza inaelezea kwa kifupi kuhusu Tanzania, biashara na haki za binadamu na uandaaji wa ripoti. Sura ya Pili inahusu uzingatiaji wa sheria na viwango vya kazi katika sekta ya biashara, ikijikita zaidi kwenye makampuni; huku Sura ya Tatu inaangalia utwaaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji, ikiangalia zaidi masuala ya fidia na uelewa kuhusu haki za ardhi. Sura ya Nne inahusu ulipagaji kodi wa makampuni katika sekta ya biashara. Sura ya Tano inaangalia uwajibikaji wa makampuni kwa jamii na jukumu la makampuni kuheshimu haki za binadamu. Sura ya Sita imejikita katika ubaguzi wa kijinsia na aina nyingine za ubaguzi katika sekta ya biashara, huku Sura ya Saba ikiangalia utendaji na ufanisi wa mamlaka za usimamizi na udhibiti katika sekta ya biashara. Sura ya Nane inatoa majumuisho na mapendekezo.

Soma hapa Muhtasari wa Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara 2017