LHRC HQ: Justice Lugakingira House
+255 22 2773038 / +255 22 2773048

RIPOTI MAALUM JUU YA MKWAMO WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

  • RIPOTI MAALUM JUU YA MKWAMO WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

RIPOTI MAALUM JUU YA MKWAMO WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA


Organization Report

Report attachment

Download

Ni takribani miaka 23 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Katika kipindi hicho chote Kituo kimekua kikiendesha programu mbalimbali za elimu ya Haki za Binadamu ikiwemo kupigania kuwepo kwa Katiba Mpya ya nchi inayoakisi maoni ya wananchi. Tanzania iliamua kuanza uandishi wa katiba mpya kutokana na kua katiba zote tano zilizopita tangu katiba ya uhuru ya mwaka 1961 mpaka katiba ya kudumu ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake yote 14 vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutoshirikisha wananchi kikamilifu. Hivyo ukaundwa mfumo ambao ungeruhusu ushiriki wa wananchi katika kupata katiba bora.

Pamoja na kukwama kwa kwa mchakato wa mabadiliko ya katiba mnamo mwezi Aprili 2015 ambao ulianzishwa mnamo mwaka 2011, bado Kituo kinaamini kuwa kuna umuhimu mkubwa na wa haraka wa kuendeleza mchakato huo kutokana na sababu mbalimbali.Kwa kutambua umuhimu huo, Kituo kimeona umuhimu wa kuandaa kitabu hiki kidogo ambacho ni zao la ripoti ya uchambuzi mkubwa wa kina uliofanywa na wataalam wa masuala ya Katiba na Sheria kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kitabu hiki kinaweka bayana mambo makuu mawili ambayo ni sababu kuu za kukwama kwa mchakato wa katiba; na mapendekezo ya njia nzuri za kuufufua na kuendeleza mchakato wa Katiba ambao unabeba maoni ya wananchi.

Ni matumaini yangu kwamba kitabu hiki kitachangia kukuza uelewa wa wananchi juu ya sababu za mkwamo wa mchakato wa Katiba na njia ambazo zinapendekezwa kuchukuliwa katika kuendeleza mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kwa kuzingatia maoni ya wananchi. Soma hapa RIPOTI MAALUM JUU YA MKWAMO WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Dkt. Helen Kijo - Bisimba

Mkurugenzi Mtendaji